Mmemhukumu na kum wua mwenye haki; yeye hakuwapinga.

Subira Na Mateso

Kwa hiyo, ndugu zangu, muwe na subira mpaka Bwana atakapo kuja. Angalieni jinsi mkulima anavyongojea ardhi itoe mavuno mazuri, jinsi anavyongojea kwa subira mvua za mwanzo na za mwisho. Hali kadhalika nanyi muwe na subira. Muwe na mioyo tha biti kwa sababu kuja kwa Bwana kumekaribia.

Read full chapter